Ofisa Habari wa Basata, Aristides Kwizela, alisema
Jokate pamoja na mbunifu mashuhuri wa mitindo ya mavazi nchini, Asia Idarous,
watatoa mada katika jukwaa hilo na watazungumzia namna ya kutumia umaarufu na
vipaji vyao kukuza kipato.
“Jukwaa hili litawataka wasanii na wadu wa sanaa
wachakarike, wapate mwanga na namna ya kutumia umaarufu na vipaji walivyonavyo
katika kuibua miradi ya ujasiriamali na kujiongezea kipato,” alisema Kwizela.
Alisema wameamua kuweka mada hiyo lengo ni wadau wa
sanaa wajifunze kutoka kwa wanamitindo hao wawili ambao wamekuwa na mafanikio
makubwa katika kazi zao zinazoendana na umaarufu wao.
0 comments:
Post a Comment