Taarifa hiyo inakuja baada ya Blatter kutangaza kuwa
atajiuzulu wadhifa wake.
Wakati ambao waendesha mashtaka nchini Marekani
wanaoifuatilia tuhuma za rushwa walikamata maafisa saba wa Fifa nchini
Switzerland kati ya watu 14 wanaotuhumiwa kwenye kashfa hiyo.
Hata hivyo Blatter alisema anatumia mamlaka
aliyopewa hata kama hayakubaliwi na kila mtu duniani.
Fifa inahitaji mabadiliko makubwa ili kukemea rushwa
Mwandishi wa BBC,Nick Bryant mjini New York anasema
kuwa bado maafisa hao wa marekani wana matumaini ya kupata ushirikiano kutoka
kwenye takwimu za Fifa kwa sasa ili kubaini namna ambavyo mzunguko wa pesa
chafu unavyomuhusisha Blatter.
Katika taarifa iliyoripotiwa kutoka kwa maafisa wa
Marekani wiki iliyopita kuhusu rushwa katika shirikisho hilo la soka
ulimwenguni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Loretta Lynch haikumshutumu Blatter
moja kwa moja .
Ingawa alisema kuwa huu ni mwanzo tu wa uchunguzi na
si mwisho.
Mwandishi wetu anasema huu ni msingi wa maafisa wa
marekani katika kuikomboa dunia katika majanga makubwa kama haya.
Mwanzoni FBI,mamlaka ya ndani ya huduma za Mapato nchini
Marekani na mwanasheria wa New York , ambaye alishiriki katika uchunguzi huo
walisema kuwa hawana maoni juu ya kujiuzulu kwa Blatter.
0 comments:
Post a Comment