Serikali
ime waagiza wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali za serikali
nchini kuwaruhusu wakaguzi wa ndani kufanya ukaguzi wa miradi ya
maendeleo hasa ile inayotekelezwa kwa ufadhili wananchi,wahisani kwa
kuwa ni sehemu ya majukumu yao.
Naibu Waziri wa Fedha ADAM MALIMA
ametoa agizo hilo bungeni alipokuwa akijibu swali lililotaka kujua
jinsi serikali kupitia vitengo vyake vya ukaguzi wa ndani katika
wizara na serikali za mitaa vinajihusisha na ukaguzi wa miradi
inayofadhiliwa na nchi wahisani.
Waziri MALIMA a mesema serikali
inafanya hivyo chini ya kitengo cha ukaguzi wa miradi mbalimbali ya
maendeleo ikiwa ni sehemu ya mpango kazi wa idara.
Aidha , amesema
katika mwaka wa fedha 2014/15 miradi ishirini na mmoja ili kaguliwa
katika m i koa ya Mtwara na Lindi kwa kushirikiana na wakaguzi wa ndani
thelathini na mbili kutoka katika halmashauri 32 za mikoa ya dare s
salaam,pwani,lindi,mtwara na Ruvuma kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Home
News
MALIMA:Wakaguzi wa ndani kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo hasa ile inayotekelezwa kwa ufadhili wananchi wahisani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment