Mwanasheria
wa Klabu ya Wafungwa yenye makao yake Mjini Ramallah, Bwana JAWAD
BOULOS amesema ADNAN amekubali kusitisha mgomo wa kula uliodumu kwa siku 55 na
anatarjiwa kuachiwa tarehe 12 mwezi jao.
Bwana
BOULOS amesema chini ya makubaliano yaliyofikiwa, Israel pia imeahidi kutomkamata
tena Bwana ADNAN kwa kile kinachofahamika kama sheria ya kuwekwa kizuizini bila
ya kufunguliwa mashitaka.
ADNAN ameshikiliwa kwa miezi 11 chini ya sheria
hiyo ambayo Israel inaitumia kuwazuia Wapalestina bila ya kuwafungulia
mashitaka na hiyo ilikuwa ni mara yake ya tisa kuzuiliwa gerezani chini ya
sheria hiyo.
0 comments:
Post a Comment