Image
Image

Pakistan imetangaza hatua za dharura kukabiliana na janga la wimbi kali la joto Kusini mwa nchi hiyo.


Pakistan imetangaza hatua za dharura kukabiliana na janga la wimbi kali la joto linaloendelea Kusini mwa nchi hiyo ambalo hadi sasa limeua 744 katika mji wa Karachi na watu 38 katika maeneo mengine.

Hatua hizo zilizotangazwa na Waziri Mkuu,NAWAZ SHARIF ni pamoja na kuanzishwa maeneo maalum yenye viyoyozi na mapanga boyi kwa ajili ya kuwaweka watu walioathirika zaidi na joto.

Hatua hizo zinakuja huku kukiwa na hasira miongoni mwa watu ambao wamewalaumu viongozi kutokana na kukatika umeme ambako kumezuia matumizi ya viyoyozi na mapanga boyi kwenye baadhi ya vituo vilivyoanzishwa kusaidia waathirika wa joto.

Vyombo vya habari vinasema vyumba vya maiti navyo vimezidiwa ng uvu ya uwezo wa kuhifadhi maiti  kufuatia ongezeko la watu wanaokufa kutokana na joto kali ambalo  sasa limefikia nyuzijoto 45 kwa  kipimo cha Centigrade sawa na nyuzijoto 113 kwa kipimo cha Fahrenheit.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment