Katika mahojiano na redio ya
Umoja wa Mataifa, msemaji wa WHO Tarik Jasarevic amesema mwaka 2012, milioni
108 za utoaji damu zimekusanywa, lakini nusu yake ilitokea kwenye nchi zenye
kipato cha juu ambapo huishi asilimia 15 tu ya raia duniani.
Bwana Jasarevic ameongeza kuwa,
utoaji damu wa kujitolea umeongezeka katika kipindi cha miongo kadhaa
iliyopita, lakini bado nchi 72 duniani hushindwa kukusanya damu kupitia utoaji
wa kujitolea na hivyo hukusanya damu kupitia utoaji wa kulipwa au familia za
wagonjwa.
Msemaji huyu amesema nchi hizo
bado zinashindwa kuhakikishia usalama wa upatikanaji wa damu, huku WHO ikieleza
kupitia taarifa yake kuwa asilimia 27 ya vifo vya wanawake wajawazito hutokea
kwa sababu ya kupoteza damu kupitia kiasi.
WHO inatoa wito kwa kila
binadamu kujitolea kutoa damu mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment