Image
Image

Viongozi wa Afrika wamekubali kupeleka wataalamu wa kijeshi nchini Burundi.


Viongozi wa Afrika wamekubali kupeleka wataalamu wa kijeshi nchini Burundi ambayo kwa karibu miezi miwili imekuwa katika machafuko ya maandamano na jaribio la mapinduzi kupinga uamuzi wa utata wa Rais PIERRE NKURUNZIZA kugombea muhula wa tatu.
Akizungumza mwishoni mwa mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika, Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja huo,SMAIL CHERGUI aliwaambia waandishi wa habari kwamba kazi ya ujumbe wa wataalamu hao 50 wa kijeshi itakuwa kuangalia nini kinachotokea na kama itahitaji kutoa ushauri nasaha kwa polisi.
Hivi sasa Bwana NKURUNZIZA anakabiliwa na shinikizo la kimataifa kufikiria upya uamuzi wake ambao wanadiplomasia wanahofu unaweza kuitumbukiza nchi hiyo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo hadi sasa machafuko ya Burundi yamesababisha vifo vya watu 40 na wengine 100,000 kukimbilia nchi jirani.
Uchaguzi wa Bunge umepangwa kufanyika tarehe 29 mwezi huu kabla ya uchaguzi wa rais mwezi ujao na tume ya uchaguzi imeidhinisha wagombea wote wanane waliojitokeza kugombea uchaguzi wa rais akiwemo Bwana NKURUNZIZA na mpinzani wake mkubwa Bwana AGATHON RWASA.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment