Mufti wa Uganda Sheikh Shaban Ramadhan Mubajje
ameitaka serikali na mashirika ya usalama ya nchi hiyo yanayochunguza mauaji ya
viongozi wa Kiislamu kufanya kazi kiuadilifu na kwa viwango vya juu vya
utaalamu.
Vyombo vya habari vya Uganda vimemnukuu Mufti wa
nchi hiyo akiitaka serikali hususan wale wanaohusika na masuala ya usalama
kutumia utaalamu wa hali ya juu katika kazi zao kama wanataka kupata ufumbuzi
wa kudumu wa mlolongo wa mauaji ya viongozi wa Kiislamu nchini humo.
Mufti Mubajje alisema hayo wilayani Kamuli mwishoni
mwa wiki wakati wa uzinduzi wa eneo la Waislamu lililojengwa na shirika lisilo
la kiserikali NGO la Kamuli Good Hope lililogharimu shilingi milioni 75.
Matamshi hayo ya Mufti Mubajje yamekuja kufuatia wimbi la mauaji ya masheikh katika mkoa wa mashariki huku mauaji ya karibuni kabisa yakiwa ni yale ya Sheikh Abdul Rashid Wafula, huko Mbale.
Matamshi hayo ya Mufti Mubajje yamekuja kufuatia wimbi la mauaji ya masheikh katika mkoa wa mashariki huku mauaji ya karibuni kabisa yakiwa ni yale ya Sheikh Abdul Rashid Wafula, huko Mbale.
Mufti Mubajje pia amewataka Waislamu wa madhehebu
mbalimbali kuungana na kuweka pembeni tofauti zao ndogo ndogo.
Amesema dini ya Uislamu inafundisha amani na kuishi
na watu kwa wema.
0 comments:
Post a Comment