Licha ya kuwepo kwa malalamiko
tangu siku ya kwanza ya zoezi hili kuanza hapa jijini Dar es Salaam lakini
mamlaka husika zimeonekana kushindwa kuyatatua matatizo hayo kwa wakati hali hiyo
inapelekea msongamano kwa baadhi ya vituo kutokupungua na watu kulazimika
kuamka usiku wa manane kuwahi namba za uandikishwaji siku moja kabla.
TAMBARARE HALISI imetembelea
vituo mbalimbali na kushuhudia wananchi wakiwa wamejipumzisha vivulini na
wengine wakichapa usingizi wakisubiri kuitwa majina huku kina mama wenye watoto
wakilalamikia kutokupewa kipaumbele.
Baadhi ya waandikishaji
waliozungumza na TAMBARARE HALISI wamedai kuwa tatizo la vidole vya baadhi ya
wananchi kutokusoma kwenye mashine limekuwa likijitokeza mara kwa mara na
kulazimika kutumia muda mwingi kuhudumia mtu mmoja hali inayozua kelele kwa
watu waliopo kwenye foleni.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi temeke
akizungumzia zoezi hilo amesema changamoto ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo
mara kwa mara ni watu kupiga simu vituoni hasa wanapoona wenzao hawafuati
utaratibu na kuongeza kuwa hakuna aliyeshikiliwa kutokana na vurugu
zinazojitokeza katika vituo hivyo.
0 comments:
Post a Comment