HUKUMU ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba,Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Gray Mgonja naWaziri wa Nishati na Madini,Daniel Yona imeahirishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam hadi jumatatu julai 6 mwaka huu.
Vigogo hawa wanakabiliwa na mashfaka ya matumizi
mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni
11.7.
Kesi hiyo iliyodumu kwa muda sasa
inayowakabili viongozi hao wazamani iko chini ya jopo la mahakimu wa mahakama
ya kisutu imelazimika kuahirishwa tena baada ya hakimu Samwek kinemela kusema
kuwa hawawezi kusoma hukumu hiyo wakati mwenyekiti wa jopo Bw.John Utamwa akiwa
anaumwa.
Kwa mara ya kwanza washitakiwa hao walifikishwa
mahakamani hapo mwaka 2008 wakikabiliwa na tuhuma hizo kutokana na kutoa
msamaha wa kodi kwa kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S ALEX STEWART ya
uingereza.
Yote tisa kumi ni julaI 6 mwaka huu ambapo
huenda jopo linalosikiliza shauri hilo likawa limekamilika na hatimaye kusoma
hukumu hiyo ambayo inasubiriwa na wengi kujua ukweli wa tuhuma zinazowakabili
vigogo hawa wa seriali ya awamu ya tatu.>>Tutakufahamisha zaidi hadi hiyo julai 6 kesi itakavyo amuliwa Endelea kutembelea Mtandao huu.



0 comments:
Post a Comment