Image
Image

Jeshi la polis lawataka wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha Sikukuu ya Eid el-Fitr


Jeshi la Polisi nchini limewataka wananchi wachukue hadhari watokapo kwenye makazi yao wakati wa Siku Kuu ya Eid el-Fitr wasiache nyumba wazi ama bila mtu na endapo italazimika ni vema watoe taarifa kwa majirani zao kwa ajili ya usalama.
Hata hivyo, jeshi hilo limewaondoa hofu wananchi kuwa, limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu limeimarisha . ulinzi kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote.
Taarifa ya jeshi hilo limewataka watumiaji wa barabara wakiwemo Maderela na watembea kwa miguu kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani, hasa kwa madereva wa magari na pikipiki,waepuke kwenda mwendo kasi na kutumia vileo wanapoendesha nyombo vyao.
Aidha, limewasisitizia wananchi kutoa taarifa haraka kwenye vyombo vya dola juu ya kitu chochote ama mienendo ya watu watakaowatilia shaka mahali popote, kwani taarifa hizo zitasaidia kuzuia uhalifu kabla haujatokea.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment