Image
Image

JK:Taifa limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza wagonjwa na vifo vitokanavyo na malaria.


Rais JAKAYA KIKWETE amesema taifa limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza wagonjwa na vifo vitokanavyo na malaria, kutokana na utekelezaji wa vipaumbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Rais KIKWETE ameyasema hayo wakati wa usinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuulia viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria kilichoko katika eneo la viwanda la TAMCO wilayani Kibaha.

Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kutumia dawa mseto kutibu wagonjwa wa malaria. kuhamasisha matumizi ya vyandarua vilivyopuliziwa dawa na kupulizia dawa inayoua mbu ndani ya nyumba.

Amesema kwa kufanya hivyo kiwango cha maambukizi nacho kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2007 hadi asilimia 10 mwaka 2012. Aidha, vifo vitokanavyo na malaria kwa wazazi vimepungua kutoka 41 kwa vizazi hai laki moja mwaka 2004 hadi 12 kwa vizazi hai laki moja mwaka 2014.

Rais KIKWETE amesema idadi ya wagonjwa wenye umri wa chini ya miaka mitano imepungua kutoka zaidi ya wagonjwa milioni tano  mwaka 2004 hadi zaidi ya wagonjwa milioni tatu mwaka 2014 na vifo vya watoto wa miaka mitano kwenda chini vimepungua kutoka zaidi ya laki saba mwaka 2004 hadi zaidi ya laki nne waka 2014.

Amesema kwa ujumla idadi ya wagonjwa wote imepungua kwa asilimia 51 na vifo kwa asilimia 71 kati ya 2004 na 2014.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment