Image
Image

Kuchelewa uandikishaji daftari la wapiga kura Pwani.


Zoezi la uandikishaji wa daftari la wapigakura baadhi ya maeneo mkoani Pwani limechelewa kuanza baada ya kudaiwa urekebishaji wa siku mbili wa mashine hizo za BVR.

Badala yake zoezi hilo kwenye kata ya vigwaza wilayani bagamoyo ambalo kwa mujibu wa tume lililotarajiwa kuanza julai 14 mkoani humo,lilitarajiwa kuanza leo huku baadhi ya makarani wakiwa hawajui hatma yao kulipwa siku hizo mbili walizocheleweshwa.

Mwenyekiti wa kijiji hicho hasani kilumbi amesema zoezi hilo kuchelewa limeharibu ratiba za wananchi wake ambao hupanga muda wa kwenda katika shughuli zao na kubaki wakisubiri kujiandikisha na huenda wengine wakakata tamaa.

Mtaribu wa zoezi hilo kituo hicho cha vigwaza Godfrey Kikolo  amekiri kuchelewa siku mbili zaidi na kusema tatizo lililopo ni mfumo wa mashine hizo kutakiwa kufanyiwa marekebisho baada ya kutumika eneo moja kwenda lingine.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment