Nyota
wa kabumbu na mchezaji mahiri wa timuya soka ya Barcelona FC awasili
nchini Gabon na kuweka jiwe la msingi katika katika uwanja wa mpira
ambapo kutachezewa michuano ya CAN mwaka 2017.
Lionel
Messi aliweka jiwe la msingi katika uwanja ambao utajengwa jijini Port-Gentil
utakao kuwa na ukubwa wakupokea watu 20,000.
Mchezaji
huyo alipokelewa kwa shangwe nchini humo ambapo rais Ali Bongo alionekana
akiendesha gari walililokuwemo huku watu wakionekana kumpongeza Lionel Messi.
Wapenzi
wa kabumbu nchini Gabon walisema kuwa ni furaha kubwa kwao kwa mchezaji
huyo kutembelea nchi yao.
Mwanamke
mmoja aliehpjiwa na shirika la habari la AFP alisema kuwa ujio wa Messi
Gabon umeleta utata.
Gabon
inahitaji kupiga vita ukosefu wa ajira na kujengwa kwa shule.
Reuters
0 comments:
Post a Comment