Waziri mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Ndugu
Edward Lowassa leo amekaribishwa rasmi kujiunga na Umoja wa Katiba ya wananchi
(UKAWA). Akiongea mbele ya waandishi wa Habari kwenye Makao Makuu ya Chama Cha
Wananchi (CUF) Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia amesema
‘tumemkaribisha Mh Lowassa kujiunga na UKAWA ili kuongeza nguvu ya kuhakikisha
tunaitoa CCM madarakani kwani tunaamini Mh Lowassa ana uwezo wa kuhamasisha
umma kuitoa CCM Madarakani katika uchaguzi mkuu ujao’. Mkutano huo umehudhuriwa
pia na Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh Freeman
Mbowe, Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba na Mwenyekiti wa NLD Mh Emmanuel
Makaidi.
Pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe,
Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh
James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD Mh Emmanuel Makaidi walipokuwa katika
mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika Makao makuu ya chama cha
Wananchi CUF, Buguruni Dar es Salaam.
Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA wakinyanyua juu mikono
kama ishara ya mshikamano katika kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment