Image
Image

Mangu athibitisha kuawa kwa watu 7 katika shambulizi kwenye kituo cha polisi stakishari ukonga jijini Dar es Salaam.


Watu saba wameuwawa kwa kupigwa risasi miongoni mwao askari polisi wanne,mtuhumiwa mmoja pamoja na raia wawili ambapo askari mmoja amejeruhiwa huku watoto wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka minne hadi mitano wakinusurika kifo katika kituo cha polisi cha sitaki shari baada ya watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kuvamia kituo hicho na kuiba silaha ambazo idadi yake kamili  bado haijafahamika.

Mkuu wa jeshi la Polisi Ernest Mangu ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa jeshi hilo aliyefika katika eneo la tukio na mara baada ya kukagua na kupata maelezo ya tukio hilo ameonesha kusikitishwa na kutamka kulaani kwa nguvu zote tukio hilo huku akiongeza kuwa tukio hilo lina viashiria vya kigaidi huku akishindwa kutaja idadi ya silaha zilizoibwa kwa madai ya sababu za kiitelijensia na uchunguzi utakapokamilika taarifa rasmi itatolewa lakini akakiri kuchukuliwa kwa baadhi ya silaha.

Katika eneo hilo la tukio ambalo ulinzi ulikuwa umeimarishwa vikali na askari polisi waliokuwa na silaha nzito pamoja na mabomu ya machozi wananchi walitakiwa kukaa mbali na tukio huku wakiwa wamejikusanya katika makundi  wakiwa wanatafakari tukio hilo la aina yake ambapo badhi yao wametoa ushauri kwa jeshi la polisi ili kukabiliana na uhalifu mpya wa kuvamia vituo vya jeshi la polisi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Said Meck Sadiq aliyefika eneo hilo  ameelezea kuwa tukio hilo ni la aina yake na kutaka ushirikiano kutoka kwa wananchi kuwezesha kuwakamata wahalifu hao huku akiongeza kuwa nyakati za kuaminiana zimeanza kutoweka na hivyo ni vyema kuwatilia mashaka hata wale wanaoonekana kwenda katika nyumba za ibada kwa kuwa mipango ya uhalifu baadhi yake husukwa na kupangwa kwenye nyumba hizo za ibada.

Tukio hilo ambalolimeshtua watu wengi jijini Dar es Salaam na maeneo mengine na linalo tafsiriwa kuwa ni lakinyama na haijapata kutokea Tambarare Halisi imeshuhudia Damu,Maganda ya Risasi pamoja na visu ambapo mashuhuda wamesema kuwa mmoja wa mtuhumiwa aliyeuwawa amepigwa risasi na majambazi wenzie baada ya pikipiki aliyokuwa akiitumia kushindwa kuwaka ili kuondoka katika eneo la tukio baada ya kutekeleza uhalifu huo ambapo watoto watatu waliofahamika kwa majina ya Lea,Recho na Richard waliokuwa wamehifadhiwa katika kituo hicho baada ya kupotea wakinusurika.
Kwani hadi sasa hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo japo Bwana Mangu kusema kuwa ni mapema mno kusema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kigaidi.

Hii si mara ya kwanza kwa kituo cha polisi kuvamiwa,mwaka uliopita kundi la watu waliokuwa wamejihami lilivamia kituo cha polisi na kukimbilia mwituni hali hii ambayo imeanza kuogofya na haswa ikizingatiwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Imefika sasa wakati kwa jeshi la polisi kuweza kuanza sasa uchunguzi wenye tija na usio na kikomo ili kubaini mizizi ya watu hawa wanao fanya matukio haya kuwa wapi wanatoka,Wanatumwa na nani,Nini dhumuni la Matukio hayo,ili ifikie wakati sasa kwamba nchi yetu inakuwa salama bila ya kutokea kwa matukio haya ambayo hayana nia njema yanaondoa roho za watu wasio na Hatia tena walinzi wataifa.
Ushauri kwa jeshi letu la Polisi ijaribu kusoma mbinu mbali mbali za watu wanaofanya uhalifu huu na ifikie wakati wasogeze urafiki na jamii kwani watu hawa pasi na shaka huenda wakawa wanatoka miongoni mwa jamii na kutekeleza unyama huu ambao bado haujafahamika nini dhumuni lao hadi hivi tena ikifanya unyama huu kwa askari wetu wenye nyenzo za kujihami  Je Siku wakigeuza kibao na kuingia kukabiliana na jamii wasio na nyenzo hali itakuwaje,NINI KITATOKEA NA athari yake?.ni swala zito wananchi na jeshi la Polisisi Kuweni Pamoja ili kusaidia kumaliza watu hawa wanao fanya unyama huu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment