Maofisa wa afya nchini Sierra Leone wametahadharisha uwezekano wa kutokea maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola.
Maofisa wa afya nchini Sierra Leone wametahadharisha uwezekano wa
kutokea maambukizi zaidi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola ikiwa ni mwaka
mmoja tangu mgonjwa wa kwanza kubainika nchini humo. Wamesema kuwa hofu
ya baadhi ya watu kukataliwa na kutengwa na jamii ni moja ya sababu
inayochangia kuenea kwa maambukizi hayo kwani wengi hujificha
wanapokumbwa na ugonjwa huo. Hata hivyo kumekuwa na kasi ya kupungua kwa
maambukizi ya ugonjwa huo katika siku za hivi karibuni ,japo kuwa
katika makao makuu ya nchi hiyo Freetown hivi karibuni kumekuwa na
maambukizi mapya ya ugonjwa huo. Zaidi ya watu 4000 walikufa kutokana na
ugonjwa wa Ebola nchini Liberia na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa moja
ya nchi tatu zilizoathirika na Ebola,zikiwemo Guinea na Liberia.
0 comments:
Post a Comment