Kwa mujibu wa Bwana Jackson
Lyamuya ambaye naye alikuwa yupo kwenye foleni kusubiria kuandikishwa amesema
kuwa katika kituo cha Midlendi Kimara Bonyokwa awali kulikuwa na mashine Moja
iliyokuwa ikifanya kazi ikaharibika tume ya taifa ya uchaguzi ikalazimika
kupeleka Mashine nyingine moja jumla zikawa mbili ambapo cha kushangaza mashine
hizo zimefanya kazi kwa muda mfupi hivyo nazo zikaharibika.
Amesema zoezi hilo ambalo
linaonekana kusuasua maeneo mengi na ikizingatiwa muda wa kuandikishwa
uliowekwa na tume ni mfupi ipo haja tume ya uchaguzi kuangalia namna gani
mashine zitafanya kazi bila kusuasua,ambapo katika kituo hicho cha Bonyokwa
baadhi ya wananchi walilazimika kubeba magodoro yao na kulala kituoni hapo ili
kupata foleni ya kuweza kuandikishwa lakini bado ikawa si kitu kwa kuwa Mashine
hizo zimekuwa zikisumbua na kuharibika.
Kutokana na kuharibika kwa
mashine hizo wananchi walilazimika kupaza sauti zao kujua nini mustakabali wa
zoezi hilo huku wakionekana wenye kujawa na jaziba kwa walicho eleza kuwa
wamelala kituoni hapo lakini hakuna ambacho kimeendelea ndipo Jeshi la Poisi
likalazimika kuingilia kati kutuliza fujo hizo.
BVR-BOKO.
Boko napo hali imeelezwa kuwa
tata katika uandikishwaji ambapo mashine za BVR mbili zilizoletwa eneo hilo
ziliharibika,huku wananchi hao wakisema kuwa wamefika kituoni hapo tangia saa
kumi na mbili asubuhi lakini bado hakuna mafanikio yeyote.
ENDELEA KUTUFUATILIA KATIKA TAARIFA ZETU,LIKE HAPO JUU ILI UWE WA KWANZA KUPATA HABARI ZETU.
0 comments:
Post a Comment