Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irine Isaka, akifungua warsha hiyo
Na K-VIS MEDIA
MFUKO wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umekutana
na Wahariri wa vyombo vya Habari Nchini, kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar
es Salaam, Julai 22, 2015, kwa nia ya kujitambulisha na kuelezea mikakati yake
ya kiutendaji na majukumu iliyo nayo.
Akiwasilisha mada kwa Wahariri hao,
Mkurugenzi Mkuu wa Kwanza wa Mfuko huo, Masha Mshomba, amesema, Mfuko huo
umeanzishwa ili kutekeleza sheria ya fidia kwa wafanyakazi (Sheria namba 20, ya
mwaka 2008.
“Majukumu ya Mfuko huu ni kuwasaidia
wafanyakazi wanaoathirika kuweza kurudi kazini au kushiriki katika shughuli
nyingine zitakazowapa kipato.” Alisema Mshomba na kuongeza kuwa majukumu
mengine ni pamoja na kutunza kumbukumbu za matukio ya ajali, magonjwa na vifo
vinavyotokana na kazi, ikiwa ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu kazi za mfuko
na manufaa yake
Alisema, Mfuko huo ni mpya na kwamba
unahitaji ushirikiano wa dhati kutoka vyombo vya habari na ndio maana Mfuko
umeona umuhimu wa kukutana na Wahariri wa vyombo vya habari kwani wao ndio
kiungo kati ya Mfuko na Umma.
Akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irine Isaka,
amesema, Mfuko huo umekuja kurahisisha ushughulikiwaji wa malalamiko ya fidia
kwa wafanyakazi moja kwa moja bila ya kuanza kupitia sehemu nyingine.
Alisema, SSRA kama mama wa Mifuko yote,
inao wajibu wa kuisaidia WCF katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria na
Wahariri wa vyombo vya Habari ni kiungo muhimu katika kuhakikisha umma wa
Watanzania unajua shughuli na kazi za Mfuko huo.
Naye kwa upande wake, Katibu wa Jukwaa
la Wahariri, Neville Meena alishukuru WCF kwa kuwaalika wahariri ili kuwaeleza
vema shughuli na majukumu ya Mfuko huo kwani vyombo vya habari ndio wakala wa
Umma na taasisi za kutoa huduma kama WCF.
Ninawapongeza WCF kwa kuwa majasiri wa
kuwaalika wahariri na kukutana nao na kupokea maswali yao, kwani taasisi
nyingine huogopa kufanya hivyo tena katika hatua ya awali kama yenu. Alisema
Meena
Mhariri Shemax Ngahamera akizungumza kwenye warsha hiyoMhariri wa vipindi wa ITV/Radio One, Steven Chuwa, (kulia), na Mhariri Mtendaji wa EFM, Scolastica Mazula, wakipitia mada zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
Mhariri Mshiriki wa gazeti la Nipashe, Ramadhan Mbwaduke, akiuliza swali
Mhariri gazeti la Serikali, Sunday News, Ichikaeli Maro, akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Baadhi ya Wahariri wakinukuu yaliyokuwa yakielezwa kwenye warsha hiyo.
Mhariri Anold Victor, akiuliza swali
Mhariri mkongwe, Mzee Yasin Sadick, akifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye warsha hiyo.
Baadhi ya Wahariri, wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa juu ya kazi na huduma zitolewazo na WCF.
MKURUGENZI Mkuu wa kwanza wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, akiwasilisha mada wakati wa warsha iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa Wahariri kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Julai 22, 2015.
Mhariri wa kujitegemea Mzee Wence Mushi akiuliza swali
0 comments:
Post a Comment