Image
Image

Mshambuliaji nguli wa Uruguay Ghiggia aliyeifungia timu yake goli la ushindi amefariki dunia.

Mshambuliaji nguli wa Uruguay Alcides Edgardo Ghiggia ambaye ndiye aliyeifungia timu yake goli la ushindi dakika 10 kabla ya mchezo kwisha katika michuano ya kombe la Dunia mwaka 1950, amefariki dunia.
Ghiggia mchezaji pekee aliyekuwa amesalia hai kati ya wachezaji wote wa kikosi cha kombe la dunia kilichoishinda Brazill mwaka 1950,ambapo dakika za lala salama zilizmuingiza katika historia ya kuipatia ushindi Uruguay.
Mchezaji huyo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 ambaye kifo chake kinatajwa kuwa ni pigo kubwa kwa Urguay kwa kuondokewa na mtu mhimu katika historia ya soka nchini humo.
Ghiggia amefariki wakati taifa hilo likiadhimisha kumbukumbu ya miaka 65 tangu kufanyika kwa fainali hizo za kombe la dunia mwaka 1950 ambapo Uruguay kupitia goli ilishinda.
Ikumbukwe kwamba katika historia ya uwanja wa Maracana ni watu watatu tu waliofanikiwa kuunyamazisha uwanja huo,na nzi za uhai wake Ghiggia alinukuliwa akiwataja watu hao kuwa ni Papa,Muuimbaji Frank Sinatra na yeye mwenyewe.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment