Image
Image

News Alert:Mgamba Awa Mkurugenzi Mpya kampuni ya The Gardian Ltd.


Mkurugenzi Mpya wa kampuni ya The Guardian Richard Mgambwa akionekana hapo baada ya kukabithiwa ofisi hivi leo.
Na.Msakanoti Manoti/Dar es Salaam.
Kampuni ya The Guardia LTD hii leo imeweza kupata mkurugenzi Mtendaji mpya Bwana Richard Mgamba hatua ambayo imepokelewa vyema na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mapema leo Shughuli hiyo ya kumpata Mkurugenzi huyo mpya Bwana Mgamba  baada ya kiti hicho kuwa wazi kwa muda baada ya Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni Hiyo Kustaafu Bwana Kiondo Mshana mwishoni mwa  mwaka jana 2014 imefanywa na mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dakta.Reginard Mengi katika ofisi hizo za the Guardiani mikocheni  jijini Dar es Salaam.
Shughuli ya kukabidhi ofisi hiyo imefanywa na Mkurugenzi mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhavile ambaye ndiye aliyekuwa ameshika nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi sita yaani kuanzia mwezi january hadi june 2015 kabla ya kuteuliwa kwa mkurugenzi mpya huyu Bwana Richard Mgamba anayeanza kazi rasmi hivi leo.

Mkurugenzi mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhavileakiwa katika ofisi za Guardian Baada ya Kumkabidi Bwana.Richard Mgamba ofisi ilikuendelea na majukumu.
Wakizungumza mara baada ya mkurugenzi mpya kukabidhiwa ofisi na kuanza kazi mara moja, baadhi ya viongozi wa kampuni ya The Guardian LTD wamesema kuteuliwa kwa Bwana.Mgamba kuwa Mkurugenzi mtendaji wa The Guardian itasababisha kampuni hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi kutokana na uwezo mkubwa wa mkurugenzi huyo na hivyo imani waliyokuwa nayo ni kubwa.

Kwa upande wa wafanyakazi wa kampuni ya The Guardian LTD Wameieleza Tambarare Halisi kuwa wamepokea kwa mikono miwili uteuzi wa mkurugenzi huyo Bwana.Richard Mgamba kutokana na ukweli kwamba ni mwenye uwezo wa kung”amua mambo haswa kwa ustadi mkubwa na ikiwa kavitumikia vyombo hivi vya habari kwa muda mwingi hivyo analojicho la kipekee la kuhakiki kuwa kampuni hiyo inapaa zaidi na zaidi na inaendelea kuwa na heshima hivyo ushirikiano watamuonyesha kwa kiwango kikubwa katika utendaji kazi wake.

Wafanyakazi wa The Guardian wakibadilishana mawazo na Mwenyekiti Mtendaji Mpya Bwana Richard Mgamba ofisini hapo baada ya kukabithiwa ofisi Rasmi ili aanze kazi.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo mpya wa The Guardian Bwanana Mgamba ambaye Tambarare Halisi ilitaka kufahamu mapokeo ya ukurugenzi huo nay eye namna alibvyo jipanga lipoje?.

Bila hata kumumunya maneno amesema kuwa”Nitafanya kazi kwa ustadi wa hali ya juu kwa nafasi hii niliyo aminiwa na kupewa hivi leo na naanza kazi rasmi hivyo imani yangu ni kuhakikisha Kampuni hii inasonga mbele zaidi na vuilevile kuhakikisha kazi inafanyika kwa ushirikiano uliyo thabiti kwani wafanyakazi na viongozi wameonyesha imani kwangu”Alisema Mgamba.

Bwana Mgamba kabla ya kujiunga na Guardian Amekuwa Mhariri Mtendaji katika gazeti la Citizen linalotolewa na Mwananchi Communications.

Baada ya Hafla hiyo fupi ya kupewa na kukabidhiwa kiti alichokuwa awali anacho Bwana Kiondo Mshana kabla ya kustaafu na kupewa Mkurungenzi Mtendaji ITV/Radio one Joyce Mhavile ambaye alikuwa kashika ofisi hiyo  kwa muda Tambarare Halisi imeshuhudia Nyuso za Furaha kwa wafanyakazi waliokuwapo eneo hilo huku kwa nyakati tofauti kila mmoja akimzungumzia Bwana Mgamba kwamba sasa wamepata chaguo zuri na ambalo kila mmoja ameliafiki bila kung”ata maneno hivyo safari itakuwa njema kwao na itakayo fanya kazi iende sawa bini sawia, kwakuwa ni mtu ambaye ataleta mabadiliko makubwa katika ya kampuni na tasnia ya habari hapa nchini kiujumla bila ya kupepesa macho.
#Hii ni sehemu ya #viongozi na wafanyakazi wakieleza walivyo mpokea #Tizama.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment