Image
Image

Nilichukulia poa leo hatunaye Banza Stone-Z Anto.

Msanii Z Anto ambaye alishawahi kutamba na ngoma kama Mpenzi jini na Binti kiziwi amefunguka na kusema kuwa aliposikia Banza Stone ni mgonjwa alichukulia poa kwa kujua ni ugonjwa wa kawaida tu anamsumbua lakini akadai alipata kuona moja ya Video yake iliyorekodiwa siku za karibuni wakati amelazwa hospital ndipo alipoamini kuwa kweli Banza Stone ni mgonjwa, Z Anto amesema hayo alipokuwa anahojiwa na East Africa Radio kwenye Planet Bongo.
"Nilipoiona hiyo video hali ya Banza Stone ilikuwa ni dhaifu sana kwa kumuona tu aligundua kweli Kaka Banza Stone anaumwa na hiyo hali ilikuwa inanipa wasiwasi juu ya afya yake lakini nilimuachia Mungu, saizi naposikia taarifa kuwa amefariki naumia ila sina namna tena nazidi kumuombea kwa Mungu ampumzishe mahali salama". alisema Z Anto
Banza Stone alishazushiwa kifo mara kadhaa na wiki kadhaa zilizopita aliweza kuongea na waaandishi wa habari na kusisitiza kuwa bado yu mzima ingawa alikiri kuwa ni mgonjwa sana na kuwaomba watanzania kumuombea ili aweze kurejea katika hali yake ya zamani, mpaka leo umauti ulipomkuta akiwa nyumbani kwao.
Ikumbukwe Banza Stone alikuwa akisumbuliwa na Fangasi za kichwa ugonjwa ambao ulifanya kulazwa ndani zaidi ya miezi kadhaa kabla ya kukutwa na umauti huo.
Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali salama Banza Stone
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment