Image
Image

Serikali yaiweka TABOA njia panda.

KITENDO cha serikali kupandisha kodi ya mabasi kutoka asilimia 10 hadi 25, kimezua sintofahamu kwa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) na hata kutishia kugoma.
Wakizungumza leo jijini Dar es Salaam, katika mkutano mkuu wa mwaka wa TABOA, wajumbe wa chama hicho wamesema, wameshangazwa na hatua ya serikali kupandisha kodi kwa sababu hawakushirikishwa wala kuelezwa vigezo vilivyotumika.
“Sisi tumeteseka muda mrefu. Ni miaka 35 sasa. Wamepandisha kodi bila kututaarifu wala kutupa vigezo vilivyotumika. Tukigoma tunaambiwa sisi ni vyama vya upinzani,” amesema Wilbard Mtega, Katibu Mkuu Mstaafu wa TABOA.
Aidha, wameshangazwa na serikali kufanya upendeleo katika kupandisha kodi kwa wasafirishaji ambapo kiwango cha ongezeko hilo la kodi hakijawagusa wamiliki wa maroli, Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) na Mradi wa Mabasi Yaendayo Mwendo Kasi (DART).
Akizungumzia kuhusu uamuzi wa TABOA, Katibu Mkuu wa chama hicho, Enea Mrutu amesema, “…kwa sasa mkutano bado unaendelea. Nafikiri hatua ya kwanza ni kuunda kamati itakayoenda kuonana na waziri husika ili kutatua tatizo hili.”
MwanaHALISI Online lilishuhudia wajumbe hao wakitofautiana kuhusu hatua ya kuchukua. Wengine wakiunga mkono kuipa serikali siku tano kupunguza kodi hiyo vinginevyo wafanye mgomo nchi nzima na wengine kupinga mgumo huo.
Mpaka habari hii inachapishwa, bado wajumbe hao hawakuafikiana juu ya hatua ya kuchukua kuhusu kupanda kwa kodi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment