Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi,
alisema kuwa sheria mpya ya kupambana na ugaidi iliyowekwa hailengi
kukiuka haki na uhuru wa raia.
Akitoa maelezo katika mwaliko wa futari, Sisi alisema, ‘‘Ni
lazima taifa lilindwe katika kipindi hiki cha changamoto nyingi lakini kuna
watu wasiotaka kuona mafanikio yetu.’’
Rais Sisi amekuwa akikabiliwa na shutuma kali dhidi ya
hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Mohammed Morsi nchini Misri.
Sheria mpya ya kupambana na ugaidi iliyopitishwa na
serikali ya Misri pia ilizua utata kwa kuhofia ukiukaji wa
haki na uhuru wa raia nchini.
Sheria hiyo ilikuwa ikiamrisha kukamatwa kwa mtu yeyote
anayeeneza taarifa zinazotofautiana na maelezo rasmi ya serikali kuhusu visa
vya ugaidi.
Vile vile sheria hiyo pia ilikuwa ikiwapa polisi uhuru wa
kutumia nguvu dhidi ya washukiwa hatari wa ugaidi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment