TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeweka hadharani majimbo mapya 26 ya uchaguzi baada ya kugawanywa kutokana na ukubwa.
Katika
mgawanyo huo, Jijini Dar es Salaam ni majimbo mawili pekee ndio
yaliyoguswa. Majimbo hayo ni Jimbo la Mbagala lililomegwa kutoka Jimbo
la Kigamboni na Jimbo la Kibamba lililokuwa sehemu ya Jimbo la Ubungo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa
NEC, Jaji Damian Lubuva ametaja majimbo mengine kuwa ni Jimbo la Handeni
katika Halmashauri Mji wa Handeni (Tanga), Nanyamba katika Halmashauri
ya Mji Nanyamba (Mtwara), Makambako Halmashauri ya Mji Makambako
(Njombe), Bitiama Halmashauri ya Wilaya Butiama (Mara), Tarime mjini
Halmashauri ya Mji Tarime (Mara).
Lubuva alitaja majimbo mengine
kuwa ni Tunduma lililopo katika Halmashauri ya Mji Tunduma (Mbeya),
Jimbo la Nsimbo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo (Katavi), Kavuu
Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe (Katavi), Geita mjini Halmashauri ya mjini
Geita (Geita), Mafinga mjini Halmashauri ya Mji Mafinga (Njombe).
Majimbo
mengine ni Kahama mjini Halmashauri ya Mji Kahama (Shinyanga), Ushetu
kwenye Halmashauri ya Wilaya Ushetu (Shinyanga), Nzega mjini lililopo
kwenye Halmashauri ya Mji wa Nzega (Tabora), Kondoa mjini Halmashauri ya
Mji Kondoa (Dodoma).
Mengine ni Newala mjini Halmashauri ya mji
Newela (Mtwara), Mbulu mjini Halmashauri ya Mji Mbulu (Arusha), Bunda
mji Halmashauri ya mji Bunda (Mara), Ndanda Halmashauri ya Wilaya ya
Masasi (Mtwara), Vwawa Halmashauri ya Wilaya Mbozi (Mbeya), Manonga
Halmashauri ya Wilaya Igunga (Tabora).
Majimbo mengine ni Mlimba
Halmashauri Kilombero (Morogoro), Madaba Halmashauri ya Wilaya Madaba
(Ruvuma), Ulyankulu Halmashauri ya Wilaya Kaliua (Tabora) na Mbinga
mjini Halmashauri ya Mji Mbinga (Ruvuma).
Pia, ameyataja majimbo
10 ambayo yaliyobadilishwa majina majina kuwa, Jimbo la Rugwe Mashariki
(Mbeya) na kuwa Jimbo la Busekelo, Jimbo la Rugwe Magharibi (Mbeya) na
kuwa Jimbo la Rugwe, Jimbo la Urambo Mashariki (Tabora) litaotwa Jimbo
la Urambo.
Mengine ni Jimbo la Urambo Magharibi (Tabora) na kuwa
Jimbo la Kaliua, Jimbo la Njombe Mgharibi (Njombe) na kuwa Jimbo la
Wanging’ombe, Jimbo la Njombe Kusini (Njombe) kwamba litaitwa Jimbo la
Lupembe.
Jimbo la Bariadi (Simiyu) litaitwa Jimbo la Itilima,
Jimbo la Bariadi Magharibi (Simiyu) linakuwa Jimbo la Bariadi, Jimbo la
Kondoa Kusini (Dodoma) kuwa Jimbo la Chemba.
Lubuva amesema,
ugawaji wa majimbo hayo ulizingatia vigezo muhimu vitatu ambavyo ni
wastani wa idadi ya watu, mipaka ya kiutawala na uwezo wa ukumbi wa
Bunge.
Amesema, kabla ya kuyagawa majimbo hayo na kuanzisha
majimbo mapya tume ilitembelea majimbo yote yaliyokidhi vigezo
nakustahili kugawanywa ambapo tume ilikutana na wadau.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment