Wakati chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema kikimtambulisha
rasmi aliyekuwa Waziri mkuu mstaafu kupitia chama cha mapinduzi CCM,Edward
Lowassa kuwa mwanachama mpya wa chama
hicho cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,Huku kukiwa na Minong’ono ya chini
chini kuwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambao hawakuwepo wakati wa mapokezi na
utambulisho wa mwanachama mpya ndani ya chama hicho walikasirika na kususia
sherehe hiyo hatimaye Tundu lissu ameweka bayana kuhusu suala hili.
Lissu-amesema kuwa kutokuwepo katika mapokezi ya
Waziri mkuu huyo Edward Lowassa ni kwamba kulikuwa na majukumu mengine ambayo
alikuwa akiyashughulikia lakini alikuwa mwenye kufuatilia mapokezi namna
yalivyokuwa yakiendelea na kusema ni mapokezi ambayo yalifana sana na yalijenga
historia ya aina yake kwa taifa letu hili la Tanzania.
Tangu tumepata uhuru kutoka kwa waingereza na hasa tangu tumeingia katika mfumo wa vyama vingi haijawahi kutokea katika nchi hii mtu wa aina ya Edward Lowassa akaondoka kwenye chama tawala akaenda kwenye Upinzani haijawahi kutokea unapoona yanatokea sasahivi yanakuambia kwamba hiki sikipindi cha kawaida ni kipindi cha mabadiliko.Amesema Lissu.
Kuhusu Mh.Lowassa kuitwa fisadi na wabunge wa
upinzani na hivyo kuonekana kama kusafishwa ndani ya chadema ,Lissu anasema
kuwa kuhusu hilo yeye ndiye alikuwa mwandishi mkuu wa kuandika orodha ya
Mafisadi kwa kushirikiana na Dkt.Slaa,jambo ambalo anakiri kuwa hawakudanganya
hata kidogo alisema kuwa Lowassa kwa ushiriki wake katika kashfa ya RICHMOND anafaa kuwa kwenye Orodha ya Mafisadi.
Ukisema haikuwa RICHMOND hapana ilikuwepo ilikuwa kashfa kubwa waziri mkuu alilazimishwa kujiuzulu lakini tunafahamu vilevile kwamba haiwezekani kitu kikubwa kama RICHMOND kikatokea kikafanywa na mtu mmoja waziri mkuu haiwezekanii washiriki wengine ni kinananiii???? Majibu ametupa jana. Amesema Lissu.
Haya ndio Majibu ya TUNDU LISSU kuhusu kutokuhudhuria katika hafla ya kumpokea Mh.Lowassa ndani ya CHADEMA,anaongea hapa#Bofya Kusikia,na kwa Taarifa Endelea kufuatilia Taarifa zetu kumbuka pia ku Like Page yetu hapo juu>>
0 comments:
Post a Comment