Akizungumza katika mkutano maalum
wa kuliombea taifa amani, ulioandaliwa na jumuia ya waislam ya wa Ahamadia
Kanda ya Ziwa Victoria, kiongozi mkuu wa wa jumuia hiyo, Sheikh TAHIR MAHMOOD
CHAUDHRY amesema inashangaza kuona vitendo vinavyovunja amani vinaendelea
kushamiri kwa kasi duniani hivyo viongozi wa dini wasipotilia mkazo mafundisho
na maonyo kwa waumini wao kuna hatari ya kuzuka kwa vita kuu ya tatu ya dunia.
Wakizungumzia hali hiyo, baadhi
ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa amani wamewataka viongozi wa dini ya
Kiislam kuwaelimisha Watanzania juu ya neno Jihad, kwa kuwa kwa kumekuwepo na mkanganyiko katika
tafsiri yake na kwa wakati mwingine kutishia kuvurugika kwa amani.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, ALLY NASORO RUFUNGA amesema
amani ni kiungo muhimu kinachounganisha viumbe vyote duniani huku akitoa wito
kwa viongozi wa dini ,serikali na vyama vya siasa kuendelea kuhubiri amani.
0 comments:
Post a Comment