Baadhi
ya viongozi wa dini na wananchi wamelaani tukio la askari kuuwawa na majambazi
jijini Dar es Salaam na kutoa wito kwa jeshi hilo kutawanya askari wenye
mafunzo ya kukabiliana na ugaidi kwenye vituo vya polisi ikiwa ni pamoja na
kufunga kamera maalum za ulinzi.
Kauli
hiyo ina kuja ikiwa nisiku chache kutokea kwa tukio la watu saba kuuawa kwa
kupigwa risasi miongoni mwao askari polisi wanne,mtuhumiwa mmoja pamoja na raia
wawili huku katika kituo cha Polisi StakiShari nakusababisha askari mmoja kujeruhiwa
baada ya watu wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia kituo hicho na kuiba silaha zaidi
ya 20 na kutokomea kusiko julikana hadi hivi leo.
Kauli
hiyo imetolewa na Sheikh Hemed Jalala ambapo mbali na kulaani tukio hilo amesema
ni vema jeshi hilo likaimarisha utaratibu wa polisi jamii kwa kutoa mafunzo ya
mara kwa mara ya namna ya kuwagundua watu wa baya huku akiwataka viongozi wa
dini kusimama katika nafasi zao kwa kuhubiria watu upendo ili wawe na hofu ya
mungu kuepusha majanga kama haya.
Kwa
upande wa wananchi wamevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuunganisha nguvu na
kufanya uchunguzi wa kina ili kukomesha matukio yaliyoshamiri hapa nchini la
watu wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia vituo vya polisi na kuwaua pamoja na
kupora silaha na kuongeza kuwa hali hiyo inawatia hofu wananchi.
Tukio hilo lilitokea julai 12,Ambapo Jeshi la Polisi limetangaza
zawadi nono ya shilingi Millioni 50 kwa atakaye fanikisha kukamatwa kwa
wahusika.
0 comments:
Post a Comment