Ikiwa imepita siku moja hadi hivi
leo baada ya tukio la watu saba kuuawa kwa kupigwa risasi miongoni mwao wakiwamo
askari polisi wanne,mtuhumiwa mmoja pamoja na raia wawili ambapo askari mmoja
amelijeruhiwa huku watoto wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka minne hadi mitano
wakinusurika kifo katika kituo cha polisi cha staki shari ukonga jijini Dar es
Salaam baada ya watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kuvamia kituo hicho na kuiba
bunduki zaidi ya 20 hali imekuwa tofauti kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Tambarare halisi iliyokuwa
ikizunguka huku na kule kupata lau mitizamo ya wananchi kuhusu matukio haya ya
kuvamiwa kwa vituo vya Polisi na watu ambao hawafahamiki mara moja na kupelekea
madhara makubwa Je wanafikiri nini pengine sababu ama kuna nini kati kati
hapa?.
Wakazi hawa wa jiji walikuwa na
mtizamo tofauti huku wakilaani wafanyaji wa matukio haya ambao bado kama wao
hawajafahamu wana nia gani laki pia wakasema ifike wakati jeshi la polisi na
wananchi wawe kitu kimoja katika taarifa kwani Dhana ya polisi jamii na ulinzi
shirikishi imeanza kwa muda kutofanya kazi yake kwakuwa Polisi na wananchi
wanaogopana.>>>Bofya Hapa Kuona wanacho kisema wadau hawa,Pia usisahau ku Like ukurasa wetu hapo juu**.
0 comments:
Post a Comment