Wakizungumzia
hali hiyo baadhi ya wakazi wa mpiji-magohe nje kidogo ya Dar es Salaam wamesema
hali hiyo inachagizwa na muamko mkubwa wananchi kujiandikisha huku mashine
zikiwa hazikidhi mahitaji ya wakazi wa jiji ambao asilimia kubwa hutegemea
kipato cha kila siku ambapo kwa sasa mtu
anatumia siku Tau hadi hadi Tano
kujiandikisha .
Vijana
ambao walijipambanua kuwa itakuwa mara ya kwanza kupiga kura wa dhamira ya
kuondoa au kufuta dhana iliyokuwa ikitawala majukwaa ya kisiasa kuwa vijana wanafika
mikutanoni lakini hawapigi kura huku wakilaani makundi yanayofanya biashara ya
kuuza namba katika vutuo vya kupigia kura.
TAMBARARE HALISI katika pita pita yake imebaini baadhi ya maofisa
wa tume wakipakia mashine kwenye bodaboda kutoka katika baadhi ya vituo kwa
madai ya kuharibika huku mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni ambaye pia ni msimamizi
wa zoezi hilo Eng. Musa Nati akikiri changamoto kadha kwa maelezo ya kuwa tume
ya taifa ya uchaguzi NEC itatoa mwelekeo kulingana na mahitaji ya wakazi katika
kuhakikisha kila mwenye sifa ya kujiandikisha anafanya hivyo.
Aidhaa kwa mwaka huu wa 2015 idadi ya uandikishwaji wananchi
katika daftari la Mpiga kura imeonekana kuongezeka maradufu,huku watu wengine
wakiamka usiku wa manane kwa lengo la kuwahi namba ili kupata kitambulisho
kitakacho fanya awe na sifa ya kupiga kura ifikapo Oktoba mwaka huu katika
uchaguzi mkuu wa kuchagua Madiwani,Wabunge hadi ngazi ya Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment