Zoezi la uandikishwaji wananchi katika daftari la mpiga kura
linaendelea ambapo inaelezwa kuwa baadhi ya maeneo ya vituo hivyo yameingia
dosari baada ya wananchi kustukia harufu ya Rushwa inayo tawala,kutoka kwa
mawakala wa zoezi hilo ili tu wawapitishe watu kujiandikisha ingali watu
wengine wameshinda vituoni hapo tangu usiku hadi hivi sasa hali iliyozusha
vurugu na zoezi hilo kusimama.
Jackson Lyamuya ni mmoja ya mwananchi aliyeko katika kituo
cha uandikishaji mpiga kura kimara Midlend jijini Dar es Salaam,ambapo amesema
kuwa hali si shwari kwani mashine ya uandikishaji yenyewe ipo moja hali ambayo
inafanya pia zoezi hilo kuwa gumu katika eneo hilo huku watu wakiwa ni wengi
wamejitokeza katika mchakato huo.
Wamesema kusuasua kwa zoezi hilo nidhahiri kwamba huenda hata
muda uliopangwa ukaisha bila asilimia ya watu waliowengi wakawa
hawajaandikishwa hivyo mamlaka husika iangalie namna gani itaweza kuwasaidia
ili zoezi hilo liweze kukamilika kwa wakati uliopangwa.
MZAMBARAUNI.
Vurugu zimeibuka katika kituo cha uandikishwaji wananchi
katika daftari la mpiga kura Ukonga Kituo cha Mzambarauni baada ya wananchi hao
kuwa tuhumu mawakala wa zoezi hilo kuwa wanawaingiza watu kujiandikisha kwa
kujuana tofauti na utaratibu ulivyo wa kupanga mstari na kuingia kwa kuitwa
namba.
Taarifa kutoka kwa wananchi waliopo kituoni hapo wanasema
kuwa utaratibu ulikuwa mzuri wa kuandikisha lakini mawakala wa zoezi hilo wao
wenyewe wakauvuruga kwa kua inaonekana wanaowaingiza huenda wana maslahi
nao,huku waandikishaji hao wanaonekana pia kuwa taratibu katika zoezi hilo
jambo ambalo linasababisha pia msongamano mkubwa usio wa lazima kituoni hapo.
BASIAYA
Wananchi hawa wapo katika kituo cha Boko Basiaya
wakiwa wamepanga foleni kwaajili ya kujiandikisha kwenye Daftari la mpiga kura
huku wengine wakionekana kukata tama na kukaa chini hadi hapo zamu yao itakapo
fika ili wakajiandikishe.
Wanadai licha ya kufika muda mwingi lakini waandishi wanaowasajili katika daftari la kudumu wapo taratibu mno jambo ambalo mtu mmoja hukaa zaidi ya dk 20 ndani kwaajili ya kuchukuliwa maelezo ili apewe kitambulisho.
0 comments:
Post a Comment