Image
Image

Wasanii wa tasnia ya filamu kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza kuwasili mji mkuu wa Senegal.

Wasanii wa tasnia ya filamu kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza kuwasili mji mkuu wa Senegal, Dakar kwaajili ya maandalizi ya tamasha la kila mwaka lijulikanalo kama Forum street Festival.
Kupitia tamasha kama hilo wasanii wanapata fursa kuwasilisha ujumbe uliopo mioyoni mwao na kutengeneza majadiliano yanayoangazia masuala mbalimbali katika jamii
Ni katika shule moja maarufu iliyopo kwenye kitongoji cha mji wa Dakar , madarasa ya shule hii ambapo kwa sasa yamegeuka kuwa kumbi za tamasha hilo,huku viti na meza vikiwa vimewekwa kando,vijana wamekaa chini kwa umakini mkubwa wakiendelea na michezo mbali mbali ya kuigiza.
'Jambo la kwanza kabisa muigizaji anapaswa kumjenga mhusika wake na kuelewa vilivyo malengo yake ,ili aweze kuwa mbunifu,na kuweza kuwavutia watazamaji wengi katika kazi yake hiyo ya kisanaa, ni moja ya misistizo inayotolewa katika tamasha hilo.
Tamasha hili la filamu ni mahala mhimu katika kazi za Sanaa, ambapo panasisistiza hadhira kuchukua nafasi yake vilivyo, ili kuanzisha mjadaa ndani ya mchezo kwa lengo kuangazia na kujadili masuala ya kijamii kwa mfano Unyanyasaji dhidi ya wanawake , uchafuzi wa mazingira au hata mada ambazo hupewa uzito mkubwa kama mlipuko wa ugonjwa wa Ebola hivi karibuni.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment