MASHINDANO ya Kombe la Kagame yaliyodumu kwa takribani wiki mbili
yamemalizika jana kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam huku Azam FC
ikipeperusha vema bendera ya tanzania kwa kuifunga Gor Mahia ya Kenya
mabao 2-0 na kutwaa ubingwa.
Azam imewatoa kimasomaso Watanzania kwa kuwa mashindano hayo
yalifanyika nyumbani, huku timu ya KMKM ikitolewa katika hatua ya
makundi na mabingwa mara tano wa mashindano hayo, Yanga ikitolewa katika
hatua ya robo fainali (dhidi ya Azam).
Kama kombe hilo lingechukuliwa na timu nyingine ingekuwa ni aibu kwa nchi pamoja na soka la Tanzania kwa ujumla.
Timu nyingine zilizoshiriki mashindano hayo yaliyoanza kwa kuchezwa
katika makundi matatu na nchi zilikotoka kwenye mabao ni Gor Mahia
(Kenya), Telecom (Djibout) na Khartoum-N (Sudan).
Nyingine APR (Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB AFC (Burundi), Heegan
FC (Somalia), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA
(Uganda).
Jambo Leo tunaipongeza Azam kwa kutwaa ubingwa huo ambapo imeweza
kujiandikia historia kwa kuwa mmoja wa mabingwa wake, na kuifanya
Tanzania kuheshimika katika ya timu za Afrika Mashariki na hata nje.
Kwa kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza baada ya kutolewa katika
fainali dhidi ya Yanga 2012, tunaamini kuwa inaweza kuhamasisha timu
nyingine za Tanzania kwamba inawezekana kutwaa ubingwa katika mashindano
ya kimataifa kama zitajipanga vizuri.
Kutwaa ubingwa huo ni matunda ya uwekezaji uliofanywa na wamiliki
wake kuwasajili wachezaji wenye uwezo, kuwa na benchi la ufundi lenye
wataalamu wa kutosha, uongozi mzuri na kupata sapoti ya mashabiki.
Kwa kuwa mashindano hayo yako kwenye kalenda, timu nyingine zijiandae
vizuri ili kuweza kushiriki katika mashindano yajayo kwa ushindani.
Tunalipongeza Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
(Cecafa) kwa kuweza kuiamini Tanzania na kuipa uenyeji na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuandaa na kusimamia vizuri mashindano
hayo.
Mwisho wa jambo moja ni mwanzo wa jingine, Azam isibweteke kwa kutwaa
ubingwa huo, ijipange kwa ajili ya kushiriki mashindano mengine yajayo
ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment