BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limelifungulia shindano la urembo
la Miss Tanzania baada ya kuridhishwa na mabadiliko kutoka kwa mratibu
wake Kampuni ya LINO International Agency Limited.
Awali, Basata ilifungia shindano hilo kutokana na waandaaji wake
kushindwa kukidhi vigezo zilivyowekwa na baraza hilo na hivyo kulazimika
kufungiwa kwa miaka miwili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na baraza hilo na kusainiwa na
Katibu Mtendaji wake, Godfrey Mngereza iliyataja mapungufu
yaliyobainishwa na kutakiwa kufanyiwa kazi kuwa ni pamoja na waandaaji
hao kushindwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji matukio
ya sanaa nchini.
Pia walishindwa kuwasilisha nyaraka mbalimbali za shindano lake
hususan mikataba ya washiriki huku tatu ikiwa ni kutumia mawakala
wasiosajiliwa na kupewa vibali kutoka Basata.
Mngereza alisema kuwa miongoni mwa mapungufu waratibu hao
wameyafanyia kazi ni kuanza mchakato wa usajili wa mawakala na
kurekebisha kanuni na taratibu za uendeshaji wa mashindano ya urembo ya
Miss Tanzania.
Alisema kuwa waratibu hao wamewasilisha muundo wa Kamati ya Uendeshaji wa shindano yenye muelekeo wa kuzingatia jinsia.
Katika kuboresha na kurudisha hadhi ya shindano la Miss Tanzania,
LINO International Agency Limited imepewa kibali cha muda kisichozidi
miezi minne kwa ajili ya maandalizi ya awali ikiwemo kukamilisha usajili
wa mawakala katika ngazi zote husika.
“Baraza linapenda kuwafahamisha wadau wote wa sanaa hususan wale wa
shindano la urembo la Miss Tanzania kwamba, Kampuni ya LINO imetekeleza
maagizo ya msingi iliyopewa kama masharti ya ,” alisema Mngereza katika
Mngereza.
Aliongeza kuwa, “hivyo basi baada ya kufanyia kazi changamoto
zilizokuwa zimejitokeza BASATA limeyafungulia mashindano ya Miss
Tanzania kwa masharti ya kukamilisha changamoto zilizobakia”.
Ni matarajio ya BASATA kwamba kampuni ya LINO itazingatia taratibu
zote za uendeshaji wa matukio ya Sanaa nchini na kwamba haitarudia tena
makosa yatakayopelekea kuliweka shindano hili katika hali ya kushuka
hadhi na kuzua sintofahamu katika jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Hashim Lundenga alisema
kuwa, uamuzi huo ni wa busara na anaishukuru Basata kwa kulirejesha
shindano hilo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment