Image
Image

CCM yakanusha uvumi wa habari ya mgombea wake wa urais Dkt.John Magufuli kuahidi kugawa kompyuta kwa walimu nchini.


Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifafanua jambo mbele ya  Waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu  ya Chama  hicho,Lumumba jijini Dar,kuhusiana na madai ya kauli inayodaiwa kutolewa na Mgombea wa Urais wa Chama hicho Dkt John Magufuli kuwa kupitia Ilani yake ya chama atatoa kompyuta kwa Walimu nchi nzima iwapo CCM itapita  madarakani,habari ambazo Nape amezikunusha vikali na kusema hayo ni  maneno ya uzusihi na kuwa Dkt Magufuli hajawahi kutamka maneno hayo  popote pale.

Nape Nnauye akionesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo imepitishwa jana  Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama hicho uliofanyika jana mjini Dodoma na  inatarajiwa kuzinduliwa Agosti  23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni.Nape amefafanua kuwa kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani  ya chama cha CCM,siyo ya  kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.

Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa CCM mapema leo jijini Dar.Picha na Michuzi Jr.
NA BAKARI ISSA WA GLOBU YA JAMII.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha uvumi ulioenea sehemu mbalimbali
kuwa Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama hicho,Dkt.John Pombe
Magufuli amewaahidi Walimu kuwapa Kompyuta kama CCM itapita madarakani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama
hicho,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kauli hiyo
siyo ya kweli na haikutolewa na Mgombea huyo wa Urais,Dkt.Magufuli.
Hatahivyo,Nape amesema kauli hiyo imetolewa kwa nia mbaya kuonyesha Chama cha Mapinduzi kimeanza ziara ya kampeni mapema.
Amesema watu walioinukuu kauli hiyo wamesema imetoka katika Ilani ya Uchaguzi
ya Chama hicho,Nape amesema " Ilani ya Uchaguzi ya CCM imetoka jana
Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama uliofanyika jana mjini Dodoma na
inatarajiwa kuzinduliwa Agosti  23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni,hivyo kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani yetu ya Uchaguzi,hiyo siyo ya
kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti
23" alisema na Nape kwa msisitizo.

Kuhusu msimamo wa Chama cha Mapinduzi kwa wanachama wanaohama chama hicho,Nape
amesema wanachama hao wanahama kwa mapenzi yao binafsi wengine wamehama
kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni za chama.
Source:Michuzi
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment