Image
Image

IOC yaonya wanariadha wanaotumia madawa.

Rais wa IOC,Thomas Bach amesema IOC haitamhurumia mwanariadha yeyote aliyeshinda nishani ya dunia kupitia njia isiyo halali.
Rais wa kamati ya Olimpiki duniani, Thomas Bach amesema kuwa, IOC haitamhurumia mwanariadha yeyote aliyeshinda nishani ya dunia kupitia njia isiyo halali.
Bach alikuwa akiyasema hayo punde baada ya kupokea taarifa inayoonesha kashfa ya matumizi ya dawa za kuusisimua misuli katika riadha.
Akiongea katika mkutano mkuu wa IOC huko Kuala Lumpur, rais huyo wa IOC anasema kuwa anasubiri matokeo ya kina kufuatia uchunguzi wa shirika linalodhibiti matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu- WADA.
Thuluthi moja ya wanariadha wametumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini.
Ripoti ya vyombo vya habari kutoka Ujerumani na Uingereza zinasema kuwa asilimia tatu ya washindi wa medali katika mashindano makubwa ya riadha kati ya mwaka 2001 na 2012 zilinyakuliwa na wanariadha ambao damu zao zinashukiwa kuwa na chembechembe za dawa hizo haramu.
Mkurugenzi mkuu wa zamani wa WADA Dick Pound, ameonya kuwa kutakuwa na mzozo mkubwa mno miongoni mwa wanariadha iwapo hilo litathibitishwa.
 Mkenya Rita Jeptoo aliyepigwa marufuku kwa kutumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini
Uchunguzi ulioendeshwa na gazeti la Uingereza la Sunday Times na kituo cha habari cha Ujerumani cha ARD, baada ya taarifa zilizovuja za maelfu ya matokeo ya uchunguzi wa damu kutoka kwa shirikisho hilo kuonesha kuwa mashrikisho ya riadha hayajakuwa yakiwajibika ipasavyo na mengine haswa yakificha ukweli.
Shirikisho la riadha duniani IAAF imetetea jitihada zake za kupambana na matumizi ya madawa ya kusisimua misuli kwa kuongeza idadi na ubora wa vifaa vinavyotumika kupima matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment