Wagonjwa wa kipindupindu(Picha na Maktaba).
UGONJWA wa kipindupindu umelipuka tena Dar es Salaam na kusababisha watu kadhaa kulazwa katika hospitali mbalimbali.
Wagonjwa hao wamelazwa katika hospitali za Sinza Palestina na Mwananyamala.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani, alisema wagonjwa waliothibitika
kuwa na kipindupindu na kulazwa hospitalini hapo ni wawili.
Alisema wagonjwa hao ambao ni mwanamke na mwanaume wanatoka Tandale na Mwananyamala.
Taarifa nyingine zilisema wagonjwa kadhaa wa kipindupindu wamelazwa katika Hospitali ya Palestina Sinza.
Hata hivyo, Mganga Mkuu wa hospitali hiyo hakuwa tayari kutaja idadi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.
“Sisi tunakusanya taarifa zote na kuziwasilisha wilayani…nenda huko watakupatia,” alisema mganga huyo.
Mara ya mwisho ugonjwa huo ulilipuka Dar es Salaam mwaka 2010 ambako
watu 17 walilazwa wakitokea Manispaa za Temeke, Kinondoni na Ilala.
Mara ya mwisho ugonjwa huo ulilipuka Dar es Salaam mwaka 2010 ambako watu 17 walilazwa wakitokea Manispaa
za Temeke, Kinondoni na Ilala.
kutokana na ugonjwa huo wananchi wametakiwa kuzingatia suala la
usafi pamoja na kufuata kanuni za afya ili kuepuka magonjwa ya
mlipuko,ikiwemo kipindupindu.
Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es salaam.
Judithi Kahama,imeonyesha kuwa kulipuka kwa ugonjwa wa Kipindupindu
katika jiji la Dar es salaam hivi karibuni kunatokana na baadhi
ya wananchi kushindwa kufuata kanuni za afya.
Kanuni hizo za usafi ni pamoja na kuchemsha maji ya kunywa,kunawa mikono na sabuni,kuosha matunda na kula
vyakula vya moto.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa,elimu ya afya bado inaendelea kutolewa
kwa wananchi ikiwa ni juhudi za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo pamoja
na wananchi kupata elimu ya kutosha juu ya
kujikinga.
Ugonjwa wa Kipindupindu umeripotiwa kulipuka Jijini Dar es salaam na
mpaka sasa kuna taarifa ya wagonjwa 11 kutoka katika Manispaa tofauti za
Jiji la Dar es salaam wameripotiwa kulazwa hospitalini kwa
kuugua ugonjwa huo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment