Kituo cha Polisi chashambuliwa jijini Istanbul.
Watu wawlili wanaripotiwa kuvamia na kushambulia kwa bomu kituo kimoja cha Polisi jijini Istanbul leo majira ya alfajiri na kuwajeruhi watu 10 huku 3 wakiwa ni maafisa wa polisi.
Aidha baaadaye kulikuwa na ufyatulianaji wa risasi baina ya polisi na watu hao na kusababisa mtu mmoja kufariki.
Maafisa hao wa polisi walipelekwa haraka katika hospitali ya Sultanbeyli lakini mmoja wa maafisa hao aliyekuwa na majeraha mabaya kabisa alifariki dunia.
0 comments:
Post a Comment