Naibu
waziri wa zamani wa afya na ustawi wa jamii na ambaye pia ni mwenyekiti wa
umoja wa wanawake CCM mkoa wa Tanga Dr,Aisha Kigoda pamoja na
viongozi wa CCM ngazi ya wilaya wamekiri kuwa chama cha CCM katika
uchaguzi mkuu ujao wa mwaka huu wilayani kilindi kitakuwa na wakati mgumu
kufuatia zoezi la kura za maoni kutawaliwa na viashiria vya rushwa na
kusababisha kuchaguliwa kwa wagombea ambao hawauziki kwa wananchi.
Dr.Kigoda ambaye
naye alikuwa katika mchakato wa kura za maoni jimbo la
kilindi pamoja na wenzake 16 wamedai kuwa baadhi
ya viongozi wa CCM ngazi ya wilaya ya kilindi wamekiuka taratibu za chama
hicho hivyo wao kwa kushirikiana na wananchi wameahidi kushindwa kutoa
ushirikiano kwa mshindi wa CCM katika jimbo la Kilindi kwa sababu matokeo
yaliyompa ushindi Omary Kibua yalitawaliwa na viashiria vya rushwa.
kwa
upande wa jimbo la Korogwe mjini kada wa CCM na ambaye pia ni mlezi wa wazazi
wilaya ya korogwe bwana Allen Nyangasa ametupiwa kadi 300 za wananchama wa chama
hicho wakati walipoitisha kikao cha kujadili mustakabali wa kikao cha CCM taifa
kama malalamiko ya viongozi waliowataka yamepitishwa hatua ambayo kada huyo
alilazimika kuwasihi kuwa waendelee wasubiri majibu kutoka makao makuu ya CCM
mjini Dodoma.
Kufuatia
hatua hiyo baadhi ya viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema
wilayani Korogwe wamewakaribisha wananchi pamoja na baadhi ya wagombea nafasi
mbali za ubunge na udiwani kwa tiketi ya CCM kujiunga na chama hicho
kutokana na madai pamoja na malalamiko ya wagombea na wanachama wa
chama tawala kuwa uchaguzi uligubikwa na viashiria vya rushwa.
Nimekuwekea hali ilivyohuko kilindi na mchakato mzima wa matokeo Bofya hapa kuona,Like Page yetu uwe wakwanza kupata Story zinapo nifikia.
Nimekuwekea hali ilivyohuko kilindi na mchakato mzima wa matokeo Bofya hapa kuona,Like Page yetu uwe wakwanza kupata Story zinapo nifikia.
0 comments:
Post a Comment