Image
Image

Mikakati mizuri yaleta mafanikio kwa BRN.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi  Dr. SHUKURU KAWAMBWA  amesema mafanikio yaliyopatikana katika miaka miwili tangu kuanzishwa kwa mpango wa matokeo makubwa sasa BRN yametokana na mikakati mizuri ya wizara.
Dr. KAWAMBWA ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa taasisi na idara zilizo chini ya Wizara hiyo na kusema kuwa mikakati mizuri iliyowekwa  ndio imesaidia kuleta mafanikio hayo
Naye Katibu mkuu wa wizara hiyo Prof; SIFUNI MCHOME amesema wamefanikiwa katika utekelezaji wa mpango huo ambapo mpaka sasa ujenzi wa vyuo vyuo vya ufundi unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake  Kamishna wa elimu katika wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Prof. EUSTELA BALALUSESA amesema wamefanikiwa kupiga hatua kubwa ambapo kiwango cha ufaulu kwa elimu ya msingi kimeongeza.
Mpango wa MATOKEO MAKUBWA SASA ulizinduliwa mwaka 2013 na Rais JAKAYA KIKWETE kwa lengo la kuleta mafanikio katika sekta mbalimbali.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment