Wagombea tisa kati 12 wa Jimbo la
Namtumbo wamejitokeza kupinga kurudiwa kwa upigaji wa kura za maoni upya katika
jimbo hilo huku wakimuunga mkono mgombea aliyeshinda,Bwana VITA KAWAWA.
Wagombea ubunge hao wakiwakilisha
wenzao wengine watano, wameibukia katika Ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari
Mjini Songea Mkoa wa Ruvuma, wakiwa na barua mbalimbali za malalamiko
wakiupinga uongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Namtumbo kurudia tena zoezi
la upigaji kura za maoni wakidai kura hizo zinalenga kumbemba mgombea mmoja
wapo aliyeshindwa katika mchakato huo.
Wanasema hawakubaliani na
viongozi hao wa CCM Namtumbo kulazimisha kurudia zoezi hilo ili kumpitisha
mgombea wao wanayemtaja kwa jina la EDWIN NGONYANI na kwamba wapo tayari
matokeo ya mwanzo yaendelee, ambayo
yalimpa ushindi mbunge aliyekuwa akitetea nafasi yake, VITA KAWAWA.
Katibu wa CCM Wilaya ya Namtumbo
ambaye pia ni Mkurugenzi wa uchaguzi wa wilaya hiyo, Bwana ABDULAZIZ MOHAMED
anasema hizo ni propaganda za wagombea na kwamba marudio ya uchaguzi yapo pale
pale.
0 comments:
Post a Comment