Orodha ya wachezaji watakaowania mchezaji bora wa Ulaya imepunguzwa kufikia wachezaji 3.
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo atapambana na washambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na Luis Suarez katika kutetea taji lake la mchezaji bora wa bara Ulaya.
Watatu hao ndio waliosalia baada ya orodha ya awali ya wachezaji 10 kupunguzwa.
Orodha ya 10 bora ilikuwa na wachezaji kama vile Gianluigi Buffon, Eden Hazard, Neymar, Pogba, Pirlo, Vidal na Tevez.
Katika dimba la klabu bingwa barani Ulaya msimu uliopita, Messi alifunga mabao 10 katika mechi 13 alizocheza, Ronaldo alifinga mabao 10 katika mechi 12 huku Suarez akitia wavuni mabao 7 katika mechi 10 alizocheza.
Messi alikuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji hili baada ya kushinda taji la UEFA Champions League katika msimu wa 2010-2011.
Wengine ambao wamewahi kutwaa taji hili ni Andres Iniesta wa Barcelona, Franck Ribery wa Bayern Munich na Cristiano Ronaldo.
Messi anapigiwa upato kutwaa taji hili kwa mara ya pili baada ya kuisaidia timu yake kushinda Ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Mshindi atabainika mnamo tarehe 27 mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment