Huyu ni Margaret Nalwoga, kutoka Uganda yeye anasema alipata ujasiri
katika kliniki licha ywa kwamba anaishi na virusi vya HIV lakini mtoto
wake ana afya nzuri.(Picha:WHO).
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya ukimwi
UNAIDS limezindua kitabu kipya kinachoonyesha hadithi ya akina mama 12
wanaoishi na virusi vya ukimwi, lakini wamefanikiwa kuzaa watoto ambao
hawakuambukizwa virusi vya ukimwi. Taarifa kamili na Grace Kaneiya
Lengo la kitabu hiki kinachoitwa Sura za kizazi bila ukimwi Afrika Mashariki na Kusini,
ni kuhamasisha jamii kuhusu huduma za kuzuia maambukizwi ya ukimwi
kutoka kwa mama hadi mtoto wakati wa ujauzito na miaka ya kwanza ya
mtoto.
Kwa mujibu wa UNAIDS, idadi ya wanawake wanaopata huduma za kuzuia
maambukizi haya imeongezeka sana kwa kipindi cha miaka michache
iliyopita, na kufika asilimia 88 ya wanawake wajawazito wanaoishi na
ukimwi kwenye ukanda huo.
UNAIDS imesema kuwa matokeo yake ni kupungua kwa asilimia 60 kwa
maambukizi ya watoto kutoka kwa mama kati ya mwaka 2009 na 2014.
Hata hivyo bado ni theluthi moja tu ya watoto wanaoishi na ukimwi
kwenye ukanda wa Afrika mashariki na kusini ndio wanapata matibabu, na
takwimu zinaonyesha kwamba bila matibabu wengi wao hawataweza kufikisha
umri wa miaka mitano.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment