Watu wawili walifariki dunia baada ya kuchomwa visu na majambazi siku ya Jumatatu nchini Sweden.
Polisi wamewakamata wanaume wawili ambao wanaoshukiwa kutekeleza tendo hilo.
Mauaji hayo yameelezwa kuwa ya kustaajabisha kwani chanzo cha mauaji hayo haukujulikana.
Mmoja wa washukiwa wa wauaji hao alikuwa amepata majeraha na kupelekwa hospitalini ambapo anaendelea kupata matibabu.
Maduka yalikuwa chini ya ulinzi mkali baada ya tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment