Image
Image

Waziri Mkuu wa Canada avunja bunge kufuatia maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi Oktoba.


Waziri Mkuu wa Canada Stephen Harper, ametangaza rasmi kuvunja bunge la serikali kufuatia maandalizi ya kampeni za wiki 11 kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika Okotoba 19.
Harper alitoa tangazo hilo baada ya kukutana na gavana David Johnston kutokana na maswali mengi yaliyokuwa yakiiandama serikali kuhusiana na tarehe ya kuanzishwa kwa kampeni za uchaguzi.
Akihimiza umuhimu wa kuzingatia usalama, Harper alifahamisha matumaini yake ya kutekelezwa kwa kampeni zote kwa misingi ya kisheria nchini Canada.
Harper aliongezea kusema kwamba ufadhili wa kifedha kwa ajili ya kampeni utatokea kwenye vyama vya kisiasa na wala sio kwenye raslimali za serikali au kodi za umma.
Canada itaandaa uchaguzi wa 42 wa kitaifa tarehe 19 mwezi Oktoba mwaka huu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment