Image
Image

Yanga yawatema wachezaji wake wawili wa kimataifa.

UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umewatema wachezaji wake wawili wa kimataifa, Mghana Joseph Zuttah na kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho, baada ya kuona uwezo wao hautaweza kuisaidia timu yao katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
Chanzo maalumu ndani ya klabu hiyo kimesema kuwa uongozi wa klabu hiyo umeona bora uwaondoe wachezaji hao baada ya kuona uwezo wao hauwezi kuisaidia timu yao katika mashindano yoyote.
Kilisema kuwa Coutinho amebakisha miezi sita katika mkataba wake na Yanga ambao utamalizika mara baada ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Coutinho alijiunga na Yanga msimu uliopita akiletwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbrazil mwenzake, Marcio Maximo, ameichezea timu hiyo mechi 33 na kuifungia mabao sita.
Zuttah alisajiliwa Juni mwaka huu kufuatia kupendekezwa na kocha Pluijm, lakini baada ya wiki mbili za Kombe la Kagame, uongozi umeona hana umuhimu.
Timu hiyo ya Jangwani imeamua kuwatoa wachezaji hao baada ya kutofanya vizuri katika michuano ya Kagame na kuondolewa katika hatua ya robo fainali.
Kupitia michuano hiyo wakaamua kutathmini na kuamua kuvunja mikataba yao.
Hata hivyo Jambo Leo ilimpigia Katibu Mkuu wa klabu hiyo ambapo simu yake ya mkononi iliita bila majibu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment