Viongozi wa Algeria, Niger na Chad watafanya mkutano siku ya Jumapili mjini Algiers kwa ajili ya kujadili mzozo unaoendelea Libya.
Mkutano huo unalenga kugusia masuala mbalimbali ya utatuzi wa mzozo wa Libya ikiwa ni pamoja na kuimarisha hali ya usalama katika kanda hiyo.
Mkutano huo pia unatarajiwa kuibua mbinu mpya za kutatua mzozo wa Libya kwa ushirikiano wa wizara za mambo ya nje kutoka nchi zote tatu, pamoja na kujihusisha na mazungumzo ya amani yanayoendeshwa na UN.
Mbinu hiyo mpya itaiwezesha Libya kuunda serikali ya kitaifa itakayotatua mzozo wa nchi na kudumisha amani kwa ujumla katika kanda hiyo.


0 comments:
Post a Comment