MBUNGE wa Songea Mjini ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya
Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi amesema Watanzania wanahitaji kupata Rais wa
kuwatumikia na si mfano wa rais.
Dk. Nchimbi amesisitiza kuwa Watanzania wanahitaji kuwa na rais
mchapakazi na kwenye kuwatumikia na huyo si mwingine bali ni mgombea
urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Akihutubia wananchi wa Songea mkoani Ruvuna ikiwa ni sehemu ya mikutano
ya kumnadi Dk. Magufuli, Nchimbi alisema chama chake kimesimamisha
mgombea urais hodari na mchapakazi akiahidi anatenda na wananchi wa
Songea Mjini na maeneo mengine ni mashahidi.
Alisema anamfahamu vizuri Dk. Magufuli na hana mashaka naye kwa nafasi
anayoomba na ndiyo maana anaomba wananchi wa Songea na Mkoa wa Ruvuma
wamchague mgombea urais wa CCM.
Pia, alisema siku zote yeye amekuwa mkweli na hapendi kuzungumza uongo
na anawahakikishia Watanzania Rais anayepaswa kuwaongoza baada ya Rais
Jakaya Kikwete ni Dk. Magufuli ambaye ndiyo mgombea sahihi.
“Watanzania wanahitaji Rais na si mfano wa Rais. Tumchague mgombea
urais wa CCM Dk. Magufuli kwani ni mchapakazi mahiri na ameonesha kwenye
ujenzi wa barabara nchini.
“Mwaka wa 2005 wakati nagombea ubunge alikuja Dk. Magufuli na aliahidi
ahadi ya barabara ambayo tayari imekamilika. Naomba kura zote za urais
apewe Dk. Magufuli ambaye ana kila aina ya sifa zote za uzalendo kwa
nchi yake,” alisema Dk. Nchimbi.
Dk. Nchimbi wakati wa mchakato wa kutamfuta mgombea urais wa CCM alikuwa
anamuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambao baada ya
jina la Lowassa kukatwa hakukubaliana na uamuzi huo lakini baada ya
kupatikana jina la Magufuli alitangaza kumuunga mkono kutoka na kutambua
uwezo wake.
Akizungumza zaidi sababu ya kuamini Dk. Magufuli ndiyo chaguo sahihi,
Dk. Nchimbi alisema hakuna mgombea ambaye anaweza kufananishwa na
Magufuli na kuongeza huu si wakati wa kuchagua mfano wa Rais bali
anahitajika Rais kwa ajili ya maendeleo.
“Niwahakikishie chaguo sahihi kwa nafasi ya urais ni Dk. Magufuli tu na
si mwingine. Ni hodari na mchapakazi makini anayejua wajibu wake.
Nasisitiza tunahitaji Rais na si mfano wa Rais,” alisema.
Magufuli
Kwa upande wake, Dk. Magufuli alisema kuwa anataka kuwa na Tanzania mpya
ambayo itawaunganisha Watanzania wote na si kuwabagua kwa sababu ya
itakadi ya vyama vya siasa.
Magufuli alisema kuwa Tanzania mpya ambayo anataka baada ya kuapishwa ni
kufanya kazi tu na kuongeza itakuwa mwiko kunyanyasa wanyonge ambao
wanajitafutia riziki.
Alisema yeye anagombea urais na si uenyekiti na lengo la kuomba nafasi
hiyo ni kuwatumikia Watanzania wote na si kubagua na kuongeza atakuwa
Rais atakayetumikia watu walio na dini na wasio na dini.
Akiwa anazungumza na wananchi wa Peremiho, Mbinga na Nyasa, Dk. Magufuli
alisema anaomba nafasi hiyo ili kuondoa kero zinazowakabili wananchi wa
maeneo mbalimbali.
Samia
Katika hatua nyingine, mgombea mwenza wa kiti cha urais, Samia Suluhu
Hassan, amesema sekta ya elimu itapewa kipaumbele ikiwa wataingia
madarakani baada ya kushindwa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25,
mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Bahi mjini mkoani
Dodoma, Hassan alisema kuwa sekta ya elimu itapewa nafasi ya kwanza ili
kuwaokoa wasichana na vishawishi wanavyopata hadi kusababisha kukatisha
masomo.
“Hili la wanafunzi kukatishwa masomo, nikiwa kama mzazi nitalisimia kwa
kushirikiana na Dk. John Mafuguli, ninawaahidi tutajenga mabweni ya
kuwalaza watoto wake wasichana ili waweze kupata elimu kwa faida yao na
taifa,” alisema.
Hassan alisema suala lingine litakalopewa kipaumbe baada ya kuingia
madarakani ni umeme, ambapo aliwaaimbia watawatumia na kuwahimiza
wasambazaji wa umeme vijijini (Rea), kusambaza maeneo yote yaliyosalia.
Alisema suala la umeme ni nyeti na lenye manufaa kwa wote, kwani litatoa
ajira kwa vijana na hata akina mama, hivyo litapewa msukumo mkubwa
katika utawala wao.
Kuhusu kilimo cha umwagiliaji mpunga, Hassan alisema Serikali itajenga
skimu za umwagiliaji na kuzifufua ama kuzikarabati zile zilizochakaa ili
wakulima waweze kuzitumia katika kilimo.
Alisema Serikali kwa kupitia ilani ya CCM imeahidi kujenga mabwawa
kwa ajili ya kilimo na mafugo, hivyo litasaidia kuongeza uzalishaji na
ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali.
Badwel
Mbunge aliyemaliza muda wake wa Jimbo la Bahi, Omary Badwel (CCM),
amemuomba mgombea mwenza wa nafasi ya urais, kuwasaidia sh. milioni 400
ili waweze kumalizia miradi yao.
Badwel alisema jimboni kwake amefanya mambo menvgi yakiwemo ya kusambaza
umeme, maji, kutengeneza skimu za umwagiliaji mpungu na kujenga
zahanati katika kata zote 20.
“Tumefanya mambo mengi muhimu kwa wananchi wa Bahi, lakini tatizo la
maji bado lipo na linahitaji kutatuliwa, tunakuomba ukiingia Ikulu hili
ulipe kipaumbele,” alisema.
Alisema Rais Jakaya Kikwete aliekeleza ahadi yake aliyowapa wakazi wa
Bahi wakati wa kampeni, lakini kutokana na ongezeko la watu, wameomba
kuongezwa fedha ili waweze kukidhi mahitaji yao.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment