Image
Image

Jaji mkuu wa Ghana amehutubia nchi kuhusu kashfa kubwa ya rushwa dhidi ya majaji.

Jaji mkuu wa Ghana amehutubia nchi kuhusu kashfa kubwa ya rushwa dhidi ya majaji. Ameahidi kuchukua hatua na maamuzi ya haraka kuhusu madai dhdi ya majaji 34 wanaoshukiwa kuhongwa kukiuka sheria.
Hii ni mara ya kwanza tangu taarifa ya kashfa hiyo kutokea. Jaji mkuu amezungumza hadharani. Georgina Theodora Wood amesema kuwa idara ya sheria inapitia kipindi kigumu,ambapo maadili ya kisheria yaliyowekwa na wakongwe wa sheria yametetereka. Aliwambia mawakili na majaji katika mji wa pili kwa ukubwa wa Kumasi kuwa ofisi yake haita msitiri yeyote atakaye patikana na hatia baada ya uchunguzi.
Jaji huyo mkuu pia amesema kuwa , mbali na uchunguzi huu wa karibuni kuwa kesi tatu zaidi za kuwaachisha kazi majaji wa makahama kuu watatu na idadi kubwa ya wanafanyi kazi wa Idara hiyo ya sheria.
Ameleeza kushangazwa na kufumuka kwa kashfa hii na waandishi ambavyo ameielezea kuwa imetokea katika kipindi ambacho yeye pia alikuwa anafanya ziara nchini kote kuwatahadharisha wafanya kazi katika idara ya sheria dhidi ya rushwa.
Serikali pia kwa mara ya kwanza imezungumzia swala hili. Naibu mwana sheria mkuu, Dominic Ayine ana mapendekezo ya kupugunza ulaji rushwa katika kitengo cha sheria. Amesema kuwa itakuwa lazima kwa majaji kuweza kuzingatia kifungu cha 40 ya kisheria kijulikanacho kwa jina Magna Carta kabla ya kuanza kazi.
Majaji 12 wanaochunguzwa wana mwisho wa siku leo kuwasilisha majibu kuhusu mashataka yanayowakabili. Wengine 14 kutoka mahakama za chini tayari wako kotini kupinga uchunguzi dhidi yao na hatua ya usimamishwa kazi
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment