Kocha wa Nigeria, Sunday Oliseh, amesema kwa sasa Enyema, amepata pigo kubwa na tumemruhusu kwenda nyumbani kwa misingi ya kibinadam.
Enyema alitarajiwa kusafiri Abuja siku ya Jumatatu, lakini alifutilia mbali safari hiyo.
Kipa wa timu ya Uingereza ya Wolves, Carl Ikeme, anatarajiwa kujaza pengo hilo katika mechi itakayokuwa ya kwanza katika timu hiyo ya Super Eagles.
Enyema, anayeichezea klabu ya Ufaransa ya Lille na mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha Super Eagles, alikuwa kipa wa timu hiyo wakati ilipoicharaza Chad kwa magoli mawili kwa moja mjini Kaduna mwezi Juni mwaka huu.
Misri ambayo haikushiriki katika fainali tatu zilizopita, iliishinda Tanzania 3-0 mjini Alexandria na sasa inaongoza kundi G, kutokana na wingi wa magoli.
Licha ya kuwa timu zinazoogopewa zaidi barani Afrika, Nigeria na Misri ambao ni mabingwa mara saba wa kombe hilo hawakufuzu kwa fainali iliyoandaliwa nchini Equatorial Guinea mapema mwaka huu.
Wakati huo huo, Shirikisho la mchezo wa Soka nchini Nigeria, NFF, limethibitisha kuwa Super Eagles itakwaruzana na Mena ya Jamuhuri Ya Niger, katika mechi ya kimataifa ya kirafiki tarehe 8 Septemba mjini Port Harcourt.



0 comments:
Post a Comment